Shika Swala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Simamisha Swala itimie kuanzia kipindi cha kupinduka jua wakati wa mchana mpaka kipindi cha usiku. Inaingia hapa Swala ya Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na Isha. Na simamisha Swala ya Alfajiri na urefushe kisomo chake, kwani Swala ya Alfajiri inahudhuriwa na Malaika wa usiku na Malaika wa mchana.